LIVERPOOL YAISTAAFISHA JEZI NO.20 ILIYOKUWA IKIVALIWA NA JOTA
Klabu ya Liverpool imeamua kuistaafisha jezi namba 20 iliyokuwa inavaliwa na mshambuliaji Diogo Jota aliyepoteza maisha Julai 03, 2025 kwa ajali ya Gari nchini Hispania, ambapo jezi hiyo haitavaliwa na mchezaji yeyote kwenye madaraja yote ya klabu hiyo.
Jota na kaka yake, Andre Silva, walipoteza maisha kwenye ajali ya gari huko Hispania mnamo huku majogoo hao wakipanga kuutumia mchezo wa kirafiki utakaopigwa Jumapili ya Julai 13 dhidi ya Preston kwa ajili ya kumuenzi nyota huyo raia wa Ureno.