Haliburton (25) alikumbwa na jeraha hilo katika robo ya kwanza ya mchezo wa Fainali ya 7 ya NBA dhidi ya Oklahoma City Thunder ambao ulikuwa ni wa kuamua bingwa wa Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu Marekani msimu uliomalizika hivi karibuni.

 

Katika mchezo huo, Haliburton alionekana akianguka bila kuguswa na mchezaji yeyote, kabla ya kuondolewa uwanjani huku akionekana kwua ni mwenye maumivu makali na wakati huohuo, timu yake ilipoteza kwa vikapu 103-91 na kushindwa kutimiza ndoto ya kutwaa taji la kwanza la NBA.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement