Timu ya Mpira wa Kikapu inayoshiriki Ligi ya NBA, Indiana Pacers, italazimika kucheza msimu ujao wa 2025/26 bila huduma ya mchezaji wake nyota, Tyrese Haliburton, aliyefanyiwa upasuaji wa misuli ya juu ya kifundo cha mguu wake wa kulia (Achilles tendon).