Kocha huyo amefichua kuwa John Obi Mikel, ambaye alikataa kushiriki mechi za kufuzu kwa michuano ya Olympic mwaka 2008, alihitaji ajumuishwe kwenye kikosi cha mwisho baada ya timu hiyo kufuzu. Ili kufanikisha hilo, wakala wa mchezaji huyo alidaiwa kutoa kiasi cha Euro 50,000 kama hongo ili Mikel aitwe kwenye kikosi hicho, lakini kocha Siasia anadai alikataa pendekezo hilo la rushwa.



Kauli hii ya Siasia inakuja katika wakati ambapo yeye na John Obi Mikel, ambaye alikuwa nahodha wa zamani wa Super Eagles, wamekuwa kwenye mvutano wa muda mrefu tangu kipindi cha uchezaji na ukocha wao katika timu ya taifa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement