Eberechi Eze aliwapa Gunners uongozi mapema, akimalizia kwa ustadi baada ya kugundua pasi ya kisigino kutoka kwa Myles Lewis-Skelly kufuatia kazi nzuri ya Gabriel Martinelli. Hilo lilikuwa bao la kwanza kwa Eze tangu asajiliwe na Arsenal, na likatosha kuwapa nafasi ya kudhibiti mchezo mapema.

Port Vale walicheza kwa ujasiri, wakipata nafasi ya kusawazisha kupitia mchezaji wao wa akiba Devante Cole (mwana wa mshambuliaji wa zamani wa England, Andrew Cole), ambaye alipiga shuti juu kidogo ya lango. Lakini matumaini yao yaliishia pale Leandro Trossard alipoongeza bao la pili akipokea pasi ndefu ya William Saliba. Ingawa kulikuwa na dalili ya kuotea, bila VAR kulikuwa hakuna cha kuwapunguzia machungu mashabiki wa Vale.


Kauli kutoka pande zote

Mikel Arteta (Kocha wa Arsenal):

“Kitu kikubwa kilichokuwa hatarini ni heshima yetu. Tulitaka kuhakikisha hawapati kasi. Tulipoteza udhibiti kwa muda, lakini wachezaji waliotokea benchi walituletea ushindi. Tulikuwa na vipindi tulivyotawala vizuri.”

Kuhusu Bukayo Saka:

“Tulimpangia dakika 60 pekee kutokana na jeraha lake. Atakuwa sawa kwa mechi ya wikendi.”

Kuhusu Eze:

“Ndiyo maana tumsajili, kuleta ubunifu na hatari mbele. Alipaswa kufunga mengine mawili. Ni mchezaji anayehitaji kuwa karibu zaidi na mpira, na tutaendelea kumuweka kwenye nafasi sahihi.”


Eberechi Eze (Mchezaji bora wa mechi):

“Ni hisia maalum kufunga bao langu la kwanza. Hii ni kitu nilichokuwa nakiwazia muda mrefu. Uwanja mgumu kuchezea, wapinzani wazuri. Tulihitaji bao la kwanza ili kupata mwelekeo.”


Darren Moore (Kocha wa Port Vale):

“Baada ya kufungwa mapema tulibaki na nidhamu na utulivu. Tulijaribu kushambulia zaidi dakika 20 za mwisho, ila bahati mbaya tukaruhusu bao la pili. Vijana wangu walionyesha ujasiri na walifanya klabu hii ijivunie.”


Nini kinafuata

Arsenal sasa watamenyana na Brighton kwenye raundi ya nne ya Carabao Cup, mechi itakayopigwa kwenye Emirates Stadium.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement