ZANZBAR: MECHI YA KATISHWA BAADA YA MWAMUZI KUCHEZEA KICHAPO
Mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar kati ya Kundemba na Zimamoto umeshindwa kumalizika baada mwamuzi wa pembeni kupata kipigo kutoka kwa mashabiki.
Pambano hilo lililazimika kusimamishwa na mwamuzi wa kati Mohamed Simba Khamis mnamo dakika za lala salama za mchezo kabla ya mchezo huo kumalizika. Mashabiki wa Kundemba wenye hasira kali ndio wamehusika kumpiga mwamuzi wa pembeni Almas Mohamed Almas kwa madai ya kuonewa kwenye mchezo huo.
Kundemba walikua wa kwanza kupata bao kupata Abdulhamid Juma dakika 56 kwa mkwaju wa penalti na Abdallah Iddi Mtumwa dakika ya 62. Mabao hayo yalidumu kwa dakika 11, ndipo Ibrahim Hilika akaipatia bao la kwanza Zimamoto. Mambo yalizidi kuwa magumu kwa timu ya Kundemba baada ya lango lao kuvamiwa kwa mashambulizi kama 'nyuki.
Wakati dakika zinazidi kuyoyoma Abdulhamid Ramadhan Juma aliweka mzani sawa kwa kufunga bao kwa mpira wa adhabu ambao uliwapita mabeki wa Kundemba.
Mchezo huo umeshindwa kutolewa maamuzi kutokana na kushindwa kumalizika kwa dakika zote za mchezo. Ligi hiyo itaendelea tena siku ya ljumaa Novemba 24 kati ya New City na Chipukizi katika Uwanja wa Mao A.