Licha ya Kikao cha Viongozi wa Klabu ya Yanga SC na upande wa Mshambuliaji Fiston Kalala Mayele kukaa lakini hakikufikia mwafaka juu ya kuongeza mkataba mpya kwa mshambuliaji huyo.

Uongozi wa klabu ya Yanga umeendelea kusisitiza hautaongeza ofa tena kwani ofa waliyompatia Mayele ni kubwa mnoo

Pia Uongozi wa klabu ya Yanga SC wamewapa siku tano wanaomsimamia Mayele kuamua hatma yake ndani ya klabu ya Yanga SC.

Fiston Mayele amepewa machaguo mawili, kusaini mkataba mpya kwa ofa ile ile au kumuuza nje ya nchi kwa dau la zaidi ya bilioni 2 za Kitanzania

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement