Klabu ya Yanga imewashukuru Wanachama na mashabiki wake kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa jana Machi 17 dhidi ya Azam FC na kupoteza mabao 2-1, Uwanja wa Mkapa.

"Shukrani kwa Wanachama na Mashabiki wetu kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu wa jana dhidi ya Azam FC. Tutarudi tukiwa imara zaidi"

Mastaa wa Yanga wamewashukuru mashabiki kwa kwa muitiko na kuwaomba wasichoke kuwakimbilia

"Wananchi, poleni sana kwa matokeo yetu. Hayakuwa matokeo tuliyotamani. Matokeo ya jana ni chachu ya maandalizi ya michezo ijayo. Tutarudi imara zaidi ya jana. Asanteni kwa muitikio wenu tunaomba msichoke kutukimbilia" ameandika Dickson Job

"Kuna muda lengo zuri linapita kwenye mipango mibaya…twende kazi" ameandika Mshery

"Samahani kwa kushindwa jana katika Dar es Salaam derby, hicho ndicho kinachofanya mpira kuvutia. Jana tulishinda na leo tumepoteza. Tutarudi tukiwa imara kupigania ubingwa." ameandika Pacome

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement