Klabu ya Yanga imeweka wazi kuja kitofauti katika mchezo wake wa muendelezo wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Dodoma jiji utakaopigwa Jumatano ya Mei 22 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga SC Ally Kamwe amesema kuwa wameamua kuja kitofauti kwa maana ya “Surprise” wakionyesha hadhi yao ya Ubingwa mara 30 wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

“Dodoma hawachezi tu na Yanga, Dodoma wanacheza na mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa hiyo lazima kila hatua tuwakumbushe Dodoma Jiji, tuwakumbushe Watanzania kwamba hawa wanaocheza leo ni mabingwa mara 30, mabingwa wenye hadhi ya nyota tatu, mabingwa wa muda wote kwenye historia ya Ligi kuu Tanzania Bara, Young Africans wapo Dodoma, ” Ally Kamwe.


Ally Kamwe ameelezea pia utofauti mwingine katika mchezo huo ambapo ameeleza kuwa kama ilivyokuwa katika mechi zilizopita kutoa majina ya wachezaji, katika mchezo huo wanatoa heshima kwa Benchi la Ufundi ambapo wamekuja na “GAMONDI DAY”.

“Hii mechi kama ambavyo tumekuwa tukizipa majina mechi zetu za Champions League msimu huu majina ya wachezaji, tukaenda mechi yetu ya Derby tukawapa wazee wetu, Rais wa Klabu ya Young Africans akaniambia mechi hii ya Dodoma Jiji kwa upekee wake tuifanye kuwa mechi ya kulishukuru benchi letu la Ufundi, kumpongeza sana Master Gamondi kwa kazi nzuri aliyoifanya yeye pamoja na wenzake kuhakikisha tumetetea Uchampion wetu, ” Ally Kamwe.

Kamwe ameeleza kuwa katika mchezo huo pia wamepanga itakapofika dakika ya 30 ya mchezo huo wanayanga wote watasimama kwa dakika moja na kupiga makofi ya heshima kwa Kocha Miguel Gamondi na Benchi la Ufundi sambamba na kuadhimisha Ubingwa wao wa 30.

Ally Kamwe ameongeza kuwa, Mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo siku inayofuata kwa maana ya Mei 23 watakuwa Bungeni kwa mualiko maalumu kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro ambapo Wizara ya michezo itakuwa ikiwasilisha hotuba yake

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement