Klabu ya Yanga imeanza kampeni ya kuelekea msimu ujao ikitambulika kama ”TOFALI LA UBINGWA ”


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe ameeleza kuwa lengo kubwa la kampeni hiyo ni kujijenga kuanzia sasa ili kuwa na msimu ujao ulio bora zaidi.

“Nyumba yetu ya mwaka 2024/25 imeshamalizika na sasa tunataka kujenga nyumba mpya ya Ubingwa ya 2025/26, Nyumba hii haiwezi kujengwa kwa kitu kingine isipokuwa nguvu kubwa ya Kiuchumi na ndio maana leo hii tunazindua kampeni ya Tofali la UBINGWA.

Tofali hili la Ubingwa ni Ada yako ya Uanachama Mwananchi mwenzangu na huu ndiyo wakati wa kulipa Ada zetu ili kuijenga Yanga imara, “ Ally Kmawe - Meneja Habari na Mawasiliano.

Endelea kutufwatilia #Tv3Sports Katika kisimbuzi cha #AzamTv CH 416


🔥 TV3 SPORTS – Kila Mchezo Una Maana.

🤝 Imepewa nguvu na @quantuminfinity_


#TV3Sports #UzinduziRasmi #MichezoAfrikaMashariki #BurudaniYaKweli #LiveNaTV3 #PoweredByQuantum

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement