Kimahesabu timu zote kwenye kundi hili zina nafasi ya kwenda robo fainali, Yanga sc wanahitaji ushindi kwenye mechi hii ili wajiweke kwenye mazingira mazuri ya wao kufuzu robo fainali lakini Belouizdad wao hata wakipata sare tu kwenye mchezo huu watakuwa wamejiweka kwenye mazingira mazuri kwanza watakuwa wameshaharibu mipango ya Yanga lakini pia watakuwa wamejiweka wao kwenye mazingira mazuri kwa sababu mchezo wa mwisho wanaenda kumaliza Medeama tofauti na Yanga ambao wao wanaenda kumaliza na Alahly ambayo ni timu ngumu sana, kwa hiyo kwenye huu mchezo Yanga hawana namna nyingine zaidi ya ushindi tu, Amezungumza Alex Ngereza.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement