Msimu wa mashindano ya CAF Interclub 2024/25 utaanza kwa raundi ya awali kati ya tarehe 16 Agosti hadi 18 Agosti, 2024 huku hatua za makundi zikipangwa kufanyika kati ya mwezi Oktoba hadi mwezi Desemba mwaka 2024.

Klabu ya Yanga itaanza kampeni zake za Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye raundi ya pili michuano hiyo na wataanzia ugenini huku Simba Sc ikianzia raundi ya pili ya kombe la Shirikisho Afrika nayo itaanzia ugenini.

Azam Fc itaanzia raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Coastal Union wakianzia raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika.

Azam Fc na Coastal Union wataanzia nyumbani kwenye michuano hiyo ambayo inaanza kurindima kuanzia Agosti 16 mpaka 18.

Tanzania ni miongoni mwa Nchi 12 pekee za Afrika zitakazoingiza timu nne kwenye mashindano ya CAF. Nchi nyingine ni Algeria, Angola, Ivory Coast, Misri, Libya, Morocco, Nigeria, DR Congo, Afrika Kusini, Sudan na Tunisia.

Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya awali utafanyika kati ya tarehe Julai 1, 2024 hadi Julai 20, 2024.

Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya pili utafanyika kati ya tarehe Julai 21 hadi Agosti 31, 2024.

Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya makundi utafanyika kati ya Septemba 1 hadi Septemba 30, 2024.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement