Klabu ya Yanga kulipandisha Kombe la Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuendelea kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuendelea kutangaza utalii.

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe ameeleza kuwa wanaupeleka Ubingwa wa 30 juu ya kilele Cha Mlima Kilimanjaro ili kuendelea kuutangaza vizuri zaidi Mlima huo na kuwaomba wahusika wa kulipandisha Kombe hilo kufanya kazi yao mara baada ya wao kumaliza wakiwa kileleni mwa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara 2023/24.

“Sisi kama Klabu bora ya Mpira nchi hii tumaona ili tuutangaze vizuri mlima wetu, ili tuunge juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan tuulete Ubingwa wa 30 hapa uende juu, tumeona jitihada za Mheshimiwa Rais kutangaza Utalii wetu alikuwa na majukumu lakini bado alitenga muda wake kuandaa Filamu wa Royal Tour ambayo imekuwa na mafanikio makubwa sana kwenye sekta yetu ya utalii lakini pia amekuja kuzindua Amazing Tanzania, ” Amesema Ally Kamwe – Afisa Habari Yanga SC.

“Na sisi kama Klabu ya wananchi, Klabu pendwa kabisa ya Rais wetu Samia tukasema tunajukumu la kuja kumsaidia mwanachama mwenzetu kutangaza kivutio cha mlima Kilimanjaro, sasa niwaombe ZARA TOUR sisi Yanga tulifanya jukumu letu kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi na sasa ni zamu yenu kufanya kazi yenu kombe likae juu ya kilele cha Mlima wa Kilimanjaro, ” Amesema Ally Kamwe – Afisa Habari Yanga SC.

Ally Kamwe pia ameomba Kombe hilo lipandishwe kileleni mwa Mlima Kilimanjaro ndani ya siku Tatu badala ya siku sita kama walivyoelezwa.

“Tumeomba siku tatu tulikuwa tunamaana yetu, hiyo siku tatu maana yake itakuwa June 02 maana yake siku tukiwa tunacheza Fainali ya FA wale wauza Ukwaju wanatakiwa wajue wanacheza na timu ya namna gani, wasije wakafikiri wanacheza Fainali na timu tu ya kawaida, lakini tulichagua siku tatu kwasababu huu ni Ubingwa wetu wa 30 na hii Tatu lazima tuhakikishe tunaisimamisha pale juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro, lakini hii Tatu ni maalumu kwaajili ya msimamo wa Ligi, wakati msimu unaanza maneno yalikuwa mengi sana na wapo baadhi ya wachambuzi wakasema Yanga watamaliza nafasi ya tatu, ” Amesema Ally Kamwe – Afisa Habari Yanga SC.

Ally Kamwe ameeleza kuwa kwa sasa sherehe ndio wanaanza baada ya Paredi na sasa wanapeleka Ubingwa Juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro na wakifanikiwa kuchukua Ubingwa wa FA pia watalipeleka Kileleni mwa Mlima Kilimanjaro

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement