Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema kufuzu kwa Yanga katika hatua ya robo fainali anaepaswa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba Mohammed Dewji na wa pili Club ya Simba.

“Wakati Mo anakuja kuwekeza Simba alisema vision yake ni kushinda ubingwa wa Afrika na baada ya hapo tukaanza mchakato wa kutawala soka la Afrika, wakati Mohammed Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua” Ahmed.



“Baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri, kama Simba SC na Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira, malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi, huu ndio ukweli ambao utadumu milele” Ahmed.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement