Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe amesema nafasi ya kutinga nusu fainali ipo wazi, kwani klabu yao imejadiliwa ndani na nje kama timu tishio inayoweza ikaisapraizi Mamelodi Sundowns.

"Kauli iliyosemwa na viongozi wa Yanga inaonyesha wanaheshimu wapinzani, lakini niwaambie ndugu zangu kuwaleta wachezaji kama Stephane Aziz Ki, Max Nzengeli, Djigui Diarra, Pacome Zouzoua na wengine wengi, hawakuja kushinda mechi dhidi ya Ihefu pekee," amesema na kuongeza;

"Labda niwaachie swali, mkiangalia kikosi cha Yanga kuna wachezaji wangapi ambao wanaweza wakaingia kwenye kikosi cha Mamelodi Sundowns, mkipata jibu basi mtajua Yanga itakuwa na mchezo gani dhidi yao."

Amesema hayo leo Machi 13,2024 wakati akichangia mjadala wa Mwananchi Space, uliandaliwa na Mwananchi Communications Ltd, wenye mada isemayo 'Ipi nafasi ya Simba, Yanga kwenye vita ya kusaka nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement