Yanga imeendeleza kasi ya kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kufikisha pointi 49 baada ya kuifunga Ihefu SC magoli 5-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar. 

Magoli ya Pacome Zouzoua (10) na Mudhathir Yahya (30) Aziz Ki (68), Augustine Okrah (84) na Maxi Mpia Nzengeli (85) yameifanya Yanga kuongoza kwa tofauti ya pointi 5 dhidi ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili na pointi 10 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya Tatu. 

Ihefu imebaki nafasi ya 8 katika msimamo ikiwa na pointi 23 katika michezo 20. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement