Timu ya Yanga imeendelea kukusanya pointi na kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu Bara 2023\2024 baada ya kuichapa Geita Gold Fc bao 1-0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Katika mashuti matano yaliyolenga lango la Geita ni moja tu lililoweza kuingia nyavuni, bao likifungwa na Stephane Aziz KI, akipokea pasi ya mwisho kutoka kwa Augustine Okrah.

Bao la KI limeifanya Yanga kuendelea kujichimbia kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 52 ikicheza mechi 19, zaidi ya pointi 8 kwa timu inayoshika nafasi ya pili Azam FC ikicheza mechi 20.

Hadi sasa KI anaongoza msimamo wa wafungaji Ligi Kuu akiwa na mabao 13, akifuatiwa na Feisal Abdala wa Azam mwenye mabao 12, Wazir Junior wa KMC akiwa na mabao 11.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement