Winga Al Ahly Hussein El-Shahat amehukumiwa kifungo nje cha mwaka mmoja na kulipa faini ya Pauni 100,000 kwa kosa la kumpiga beki wa kulia wa Pyramids Mohamed El-Chibi wakati wa kipigo cha Al Ahly cha 3-0 dhidi ya Pyramids mnamo Julai 23, 2023 msimu uliopita. Sambamba na hilo amefungiwa kujihusisha na michezo kwa kipindi cha miaka mitano.


El-Chibi alimshutumu El-Shahat kwa kumpiga makofi, matusi na vitisho mbele ya mamilioni ya watazamaji waliokuwa kwakitazama mchezo huo, mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, El-Shahat alimuomba msamaha El-Chibi ana kwa ana.

Katika hatua nyingine Shirikisho la soka Nchini Misri, (EFA) limemfungia mechi 6 mlalamikaji wa kesi hiyo Mohamed El-Chibi, beki wa Pyramids sambamba na faini ya pauni 100,000 kwa kosa la kukiuka kanuni za EFA kwa kupeleka masuala ya soka kwenye mahakama ya uhalifu.

Katika ufafanuzi wa adhabu hiyo, El-Shahat kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja atakuwa chini ya uangalizi, hatakiwi kufanya kosa lolote, aidha ndani ya kipindi cha miaka mitano Shahat hataruhusiwa kushika wadhifa wowote wala kuwa mwanachama wa timu yeyote ya michezo na hatma yake itasalia kwenye uangalizi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement