Nyota chipukizi Wilfried Nathan Douala ambaye aliwavutia wengi baada ya kuitwa katika kikosi cha Cameroon kilichoshiriki Afcon iliyoisha Ivory Coast, amepatikana na kashfa ya udanganyifu wa “umri wake” na utambulisho mara mbili.

Shirikisho la Kandanda Cameroon (Fecafoot) limetangaza kupitia vyombo kadhaa vya habari nchini humo, kumfungia Douala akiwa ni katika orodha ya wachezaji 62 waliozuiwa kucheza mechi za mchujo kombe la Mtn Elite One nchini humo.

Hii si mara ya kwanza kwa Cameroon kukumbwa na sakata la udanganyifu wa umri.

Mnamo Januari 2023, Shirikisho la Soka la Cameroon lililazimika kuwatoa wachezaji 21 kati ya 30 wa timu ya taifa ya wachezaji wasiozidi U17 iliyochaguliwa kwa mashindano ya kufuzu Afcon U-17, baada ya uchunguzi wa MRI ili kubaini umri wao halisi kupitia mifupa kuonyesha walidanganya.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement