Uhispania itakutana na mwenyeji Ufaransa katika fainali ya mashindano ya Soka ya wanaume ya Olimpiki baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Morocco.

Washindi wa medali za fedha za 2020 walibaki nyuma katika kipindi cha kwanza cha nusu fainali baada ya mfungaji bora wa michuano hiyo Soufiane Rahimi kufunga penalti kwa bao lake la sita kwenye Michezo hiyo.

Fermin Lopez wa Barcelona alisawazisha katikati ya kipindi cha pili mjini Marseille baada ya kuuwahi mpira uliolegea kwenye eneo la hatari.

Juanlu Sanchez ambaye ni mchezaji wa akiba kisha alifunga bao la ushindi dakika tano kabla ya mechi kukamilika na kuipeleka timu yake katika fainali itakayipigwa Ijumaa mjini Paris, ambapo watakutana na vijana wa Thierry Henry wa Ufaransa.

Wenyeji waliishinda Misri 3-1 baada ya muda wa ziada katika mechi nyingine ya nne-bora, Morocco itamenyana na Misri katika mechi ya medali ya shaba mjini Nantes siku ya Alhamisi

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement