WAZIRI WA UTAMADUNI GERSON MSIGWA AMEIPONGEZA TFF KWA KUWA NA UHUSIANO MZURI NA CAF PAMOJA NA FIFA
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia kwa katibu wake Gerson Msigwa amelipongeza Shirikisho la Soka nchini kwa maana ya TFF kwa kuwa na mahusiano mazuri na CAF pamoja na FIFA kwa lengo la kuendelea kukuza michezo kwa vijana.
Msigwa amezungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya mpira wa miguu kwa shule kwa maana ya Football For Schools- F4S uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kuongeza kuwa anaamini Program mpaka kufikia mwaka 2027 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa Michuano ya AFCON huo utakuwa ni ukurasa mpya wa mpira wa Tanzania kwa kutengeneza wachezaji watakaotumika kwenye AFCON 2027 na hata wabataoendelea kutumika kwa manufaa ya Taifa.