Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amelitaka Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Tanzania (TBF) liendelee kusimamia ubora na viwango vinavyoongoza mchezo huo ili uweze kuvutia uwekezaji zaidi.

Mhe. Mwinjuma ametoa kauli hiyo Machi 4, 2024 jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jezi mpya za Timu ya Taifa ya mpira wa kikapu ambapo amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya viwanja vya mpira wa kikapu vitakavyotumiwa kwenye mashindano yoyote ya kiwango cha Afrika.

“Kwa Niaba ya Serikali naahidi kuendelea kushirikiana nanyi katika kutafuta wawekezaji ili kuhakikisha mpira wa kikapu unakua Bora zaidi na kuchezwa katika viwango ambavyo Watazamaji na wapenzi wa mpira wa kikapu wangetegemea kuviona; viwango vyenye ushindani ndani na nje ya nchi ” amesema Mhe. Mwinjuma.






You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement