Katika taifa la Cameroon kumekua na mzozo ambao unaendelea kisa kikubwa ni wizara ya michezo chini ya waziri husika bwana KOMBI kuingilia mamlaka ya Shirikisho la mpira nchini Cameroon (FECAFOOT).

Bwana NARCISSE MOUELLE KOMBI ambae ndie Waziri wa michezo aliamua kumtambulisha kocha mbeligiji bwana MARC BRY kurithi mikoba ya alie wahi kua mchezaji na kocha pia RIGOBERT SONG baada ya kufukuzwa KAZI.

Hata hivyo kwa mujibu wa taratibu ni kwamba shirikisho la mpira ndilo lenye mamlaka la kutoa mapendekezo ya kocha kuchaguliwa na kuteuliwa lakini Serikali yenyewe itakua na jukumuu la kumlipa mshahara.

Sasa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Cameroon bwana SAMWEL ETOO mchezaji wa zamani wa nchi hiyo na mfungaji bora wa muda wote nchini Cameroon akiwa na magoli 56 ameonekana kuto ridhishwa na maamuzi ya waziri husika wa michezo kuto mshirikisha katika maamuzi ya kutafuta kocha mpya

Hata hivyo ETOO amekataa kumtambulisha kocha huyoo mbeligiji bwana MARC BRY na kufuatiaa sakata hilo ETOO ameonekana akizungmza na bwana KOMBI waziri akimwambia kua yeye kama waziri hapaswi kuingilia kazi ya Shirikisho inatakiwa kila MTU asimame katika mipaka yake 

Watu wanajiuliza shirikisho ipo chini ya Serikali kama ni hivyo je Serikali ina haki kufanya teuzi pasipo kuwapa taarifa shirikisho au ni mahusiano mabaya kati ya Rais wa shirikisho la mpira nchini Cameroon FECAFOOT na waziri husika wa michezo bwana KOMBI.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement