Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt: Damas Ndumbaro amezitaka Klabu za Soka nchini kuwashika mkono wadau na wawekezaji kwa kuwa na utawala sambamba na uongozi bora kwa lengo la kujikuza zaidi kiuchumi kwa maendeleo ya michezo.

Waziri Ndumbaro ameeleza hayo na kuwataka mashabiki sambamba na wanachama kusimamia nidhamu ili kuendelea kulinda heshima ya klabu husika kwa lengo la kuendelea kuwavutia zaidi wawekezaji.

Kwa upande mwingine Waziri Ndumbaro ameipongeza Klabu ya Simba kwa ubora wanaoendelea kuonyesha licha ya kutokuwa na muendelezo mzuri katika mashindano mbalimbali na kuweka wazi kuwa kwa usajili unaendelea kufanyika anaamini Ligi kuu ya msimu ujao itakuwa na ushindani wa hali ya juu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Murtaza Mangungu amewataka wanachama kuendelea kutunza nembo ya Klabu hiyo ili kuongeza zaidi wigo wa udhamini.

Naye Mtendaji Mkuu wa Simba SC Imani Kajula ameeleza kuwa wanaimani juu ya safari yao ya kujihakikishia wanakua kinara ya Ligi Afrika na kutaka kila upande ndani ya Klabu kuwajibika kwa maendeleo ya Klabu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement