Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' ameitaka Yanga ilalamikie bao la Azizi KI lililokataliwa katika mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns kwenye robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa jana Aprili 5 katika Uwanja wa Loftus Versfeld, Pretoria, Afrika Kusini.

MwanaFA ameandika katika mtandao wa X (Twitter) "Nimetoka kuongea na viongozi wa Yanga na tumekubaliana wanaiandikia CAF kulalamika kuhusiana na goli la wazi lililokataliwa. Haitabatilisha matokeo,lakini angalau tuweke kumbukumbu sawa na ikithibitika hata mwamuzi achukuliwe hatua stahiki." "LILE LILIKUWA GOLI HALALI."

Yanga wamekosa penalti tatu zilizopigwa na Stephane Aziz KI, Dickson Job na Ibrahim Bacca na waliofunga ni Joseph Guede na Augustine Okrah huku Mamelodi zikipigwa na Marcelo Allende, Lucas Ribeiro Costa na Neo Maema na aliyekosa ni Gaston Sirino.

Mamelodi anasikilizia mshindi wa mechi kati ya Asec Mimosas na Espérance Sportive de Tunis itakayopigwa leo Aprili 6 katika Uwanja wa Felix Houphouet Boigny, Ivory Coast saa 5:00 usiku.




You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement