WAZIRI NDUMBARO ABISHA HODI UWANJA WA CCM KIRUMBA KUELEKEA AFCON 2027
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekagua hali ya Uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza ambao upo kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa kwa ajili ya mashindano ya AFCON 2027
Mhe. Ndumbaro amefanya ukaguzi huo leo Julai 2, 2027 akiwa ameambatana na Mbunge wa Ilemela Mhe. Angelina Mabula ambapo amekagua eneo la kuchezea, vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji, sehemu za maliwato na eneo la watu mashuhuri.
Mhe. Ndumbaro amesema mpango wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja huo ambao utatumika kama uwanja wa mazoezi wakati wa michuano hiyo ambayo nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zitakuwa mwenyeji wa michuano ya AFCON 2027.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Angelina Mabula ameishukuru serikali kwa kuujumuisha uwanja huo katika mpango wa AFCON 2027.
Viwanja vingine vitakavyo karabatiwa ni CCM Jamhuri Morogoro, Uwanja wa Majimaji Songea Mkwakwani Tanga na uwanja wa Sokoine Mbeya.