Watu saba wamefariki na wengine 21 kujeruhiwa baada ya gari la mashindano ya mbio kuwagonga watazamaji katika hafla ya uendesdhaji magari nchini Sri Lanka.

Ajali hiyo ilitokea katika mbio za Fox Hill Supercross siku ya Jumapili huko Diyatalawa.

Miongoni mwa waliofariki ni maafisa wanne wa mbio pamoja na watazamaji, akiwemo msichana wa miaka minane, jeshi lilisema.

Maelezo machache yametolewa kuhusu dereva, hali yake na iwapo atakabiliwa na mashtaka.



Lakini mamlaka ilisema uchunguzi kamili wa polisi ulikuwa unaendelea kuhusu ajali hiyo iliyotokea kwenye njia inayomilikiwa na jeshi. Diyatalawa, katikati mwa kusini mwa Sri Lanka ni mji wa zamani unaochukuliwa kuwa ngome na jeshi lina chuo chake huko.

"Ajali hii ilitokea wakati gari liliporuka nje ya njia," msemaji wa polisi Nihal Talduwa alisema, kwa mujibu wa BBC Sinhala.

Kulingana na mashuhuda, ajali hiyo ilitokea mara baada ya gari lingine kupinduka kwenye njia.

Maafisa walijaribu kupunguza mwendo wa magari kuzunguka eneo la tukio kwa kuwasha taa za manjano, lakini magari yalipopita kwa kasi, gari moja jekundu lilitoka nje na kuwagonga watazamaji kando ya njia isiyokuwa na walinzi.








You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement