Wanariadha hao wawili wa Kenya na mmoja wa Ethiopia wako chini ya uchunguzi baada ya kushutumiwa kwa kumruhusu kwa makusudi mwanariadha wa China, He Jie, kushinda Nusu Marathon ya Beijing.

Tukio hilo, lililonekana mitandaoni kwenye video iliyosambazwa sana, ikionyesha wanariadha hao waliotambulika kama Robert Keter na Willy Mnangat kutoka Kenya, na Dejene Hailu kutoka Ethiopia wakionekana kumpisha njia He Jie.


Katika video hiyo yenye utata, wanariadha hao watatu wanaonekana wakielekeza mikono yao kwenye mstari wa mwisho na wakipunguza kasi yao ili kumruhusu He, mshindi wa medali ya dhahabu ya marathon katika Michezo ya Asia ya 2023, kuongoza na hatimaye kushinda mashindano kwa tofauti ya sekunde moja tu.

“Ilionekana kama jambo lililopangwa,” alisema mtazamaji mmoja wa mashindano hayo aliyeshuhudia tukio hilo.

Wizara ya Michezo Beijing imethibitisha kwamba uchunguzi unaendelea.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement