Mara baada ya kuhusishwa kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalez, Wadau wa Soka nchini wameweka wazi kuwa wanaamini urejeo wake utaleta mabadiliko ambayo wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wanayahitaji kwa sasa.

Wadau wa Soka hapa nchini ambapo wameongeza kuwa wanaamini atakapojerea ataendelea pale alipoishia pindi alipokuwa akihudumu ndani ya Klabu hiyo.

“Kama ni taarifa yenye ukweli inaweza kuwa Simba wamefanya kwa vitendo kwa yale ambayo wameyazungumza kuwa wanataka kufanya mabadiliko makubwa, wote tunakumbuka nyakati Barbara alikaa ndani ya Simba SC ndizo nyakati ambazo Simba waliweza kufanya vitu vingi sana na sio kwa hapa ndani pekee, ilirejesha Ufalme wake kwenye Ligi ya ndani n ahata michuano ya Kimataifa, ” Amesema Hebron Faiton – Mdau wa Soka.

Kwa upande mwingine Herbron ameeleza kuwa hata kwa upande wa usajili kwa sasa imekuwa tofauti na kipindi ambacho yupo Barbara ambap[o sajili zilizokuwa zikifanyika zilikuwa hazina lawama.

“Barbara wakati anafanya kazi Simba SC klabu haikuwa na wakati mbaya, Barbara aliweza kuipa Simba SC heshima kubwa kubwa ikiwa mfumo mzuri wa uendeshaji wa Klabu, ” Amesema Hebron Faiton – Mdau wa Soka.

Hebron ameongeza kuwa ushirikiano alioujenga Barbara dhidi ya Klabu za nje sambamba na viongozi wa CAF iliweza kuleta manufaa makubwa.

Kwa upande wake Aziz Shentembo ameeleza kuwa kwa upande wa Barbara kuhusishwa kurejea Simba SC kunaleta matumaini kwa mashabiki ambao mpaka sasa bado hawajajua ni nini kitafanyika kwa msimu ujao kwa manufaa ya Klabu sambamba na kurejesha furaha kwa mashabiki na wanachama wa Klabu hiyo.

“Kwa hali inayopitia Simba kwa sasa inaweza kufanya hizi stori zikawa kweli au sio kweli lakini kama ni kweli inaweza kuleta athari chanya kwa pande zote kwa sababu mashabiki wengi wanaamini katika mabadiliko ya viongozi, wanatamani baadhi ya viongozi wajiondoe, wengi wanaamini alivyokuwepo Barbara walikuwa wanapata kile wanachokihitaji, ” Amesema Aziz Shentembo – Mdau wa Soka.

Aziz ameongeza kuwa Klabu ya Yanga kuwa walipo ni kutokana na Rais wa Klabu hiyo Eng: Hersi kukutana na viongozi wakubwa wanatoka katika Klabu Zilizofanikiwa kitu alichokuwa akikifanya Barbara ambapo mashabiki wanaamini iwapo atarejea anaendeleza pale alipoishia.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement