WACHEZAJI WAWILI WA LIGI KUU UINGEREZA WAMEKAMATWA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI
Wanasoka wawili wa Ligi Kuu ya Uingereza wamekamatwa kwa tuhuma za ubakaji, Wawili hao, wote wakiwa na umri wa miaka 19, waliachiliwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa na polisi.
Wachezaji hao wapo katika klabu moja, ambayo ilikataa kuzungumzia madai hayo, "Maafisa wamewakamata wachezaji wawili kufuatia ripoti ya ubakaji," msemaji wa polisi alisema.
“Kijana wa miaka 19 alikamatwa kwa tuhuma za kushambulia na kusaidia ubakaji. Mwanaume wa pili mwenye umri wa miaka 19 alikamatwa kwa tuhuma za ubakaji. "Wote wawili wameachiliwa kwa dhamana ya polisi."
Madai hayo yaliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la The Sun, ambalo lilisema shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa siku ya Ijumaa.
Haijajulikana iwapo wachezaji hao wamesimamishwa kazi kusubiri matokeo ya uchunguzi wa polisi.
Ligi Kuu ilianzisha mafunzo ya lazima ya idhini ya ngono kwa wachezaji na wafanyakazi mnamo 2022 kufuatia matukio ya hali ya juu yaliyohusisha wanasoka wa daraja la juu.
Mnamo Novemba uchunguzi wa Panorama uligundua vilabu vya Ligi ya Premia viliendelea kuchezesha wanasoka wawili, huku wakijua walikuwa chini ya uchunguzi wa polisi kwa unyanyasaji wa kingono au majumbani.