WACHEZAJI WA TANZANIA WA KIKE WANAOCHEZA ULAYA
MIAKA ya nyuma ilizoeleka kushuhudia wachezaji wa kike kutoka Nigeria, Morocco, Afrika Kusini wakicheza karibu kila msimu Ligi ya Mabingwa Ulaya upande wa wanawake ni kama ilikuwa stori tu kwa wachezaji wa Kitanzania ambao msimu huu wa 2023/24, Aisha Masaka ameonyeshwa kuwa inawezekana.
Aisha Masaka (Bk Hacken Ff- Sweden). Japo alianza kwa kusumbuliwa na majeraha ambayo yalimfanya msimu uliopita kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu, Masaka amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu ambao ameingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Uefa kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa kike kutoka Tanzania kucheza michuano hiyo upande wa wanawake.
Clara Luvanga (Al Nassr- Saudia). Anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wa kike wenye vipaji vikubwa, kuna kipindi alikumbwa na matatizo (ilifichwa kumlinda) ambayo yalimfanya kushindwa kuonekana uwanjani kwa kipindi kirefu lakini wanasaikolojia walimjenga ndipo walipoibukia Hispania ambako alicheza kwa kipindi kifupi na kutua Saudia Arabia.
Enekia Kasonga (Flames-Saudia). Wamorocco wanamjua vizuri Enekia, akiwa na Ausfaz assa Zag alifunga mabao 49 kwenye michezo 41 kabla ya kwenda Saudia ambako anaichezea Eastern Flames.
Julietha Singano (Juavares - Mexico). Mwanasoka huyu alikuwa wa kwanza kuandika historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza soka la kulipwa Mexico kwa upande wa wanawake. Kucheza soka nchini humo kunaifanya Ligi ya Tanzania kujulikana kwani timu hiyo inashiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Mexico, moja ya taifa kubwa kisoka.
Opah Clement (Beskitas - Uturuki). Opah mwenye mabao tisa kwenye michezo saba ya Ligi Kuu Uturuki kwa wana-wake ni miongoni mwa mabinti wanaoiwakilisha vyema Tanzania.
Diana Msewa (Amed Spor - Uturuki). Mwanadada huyo ambaye kwa sasa anakipiga Uturuki anaongeza idadi ya wanawake Watanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.