WACHEZAJI SABA WA MAMELODI WATASAFIRI KWA NDEGE BINAFSI KUTOKA ALGERIA MPAKA TANZANIA
Mamelodi sundown imefanya maandalizi maalum ya kusafiri kwa nyota saba wa Bafana Bafana katika kikosi chao kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Young Africa nchini Tanzania wikendi hii.
Nahodha Ronwen Williams, Grant Kekana, Aubrey Modiba, Thapelo Morena, Terrence Mashego, Teboho Mokoena na Themba Zwane wako pamoja na timu ya taifa nchini Algeria katika mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa za FIFA Series 2024 na pia ni wachezaji muhimu kwa klabu yao ya mkondo wa kwanza wa robo fainali nchini Tanzania.
Kwa hivyo, taarifa zilizonifikia zinaeleza kuwa Mamelodi sundowns itawasafirisha kwa ndege wachezaji wao moja kwa moja kutoka Algeria hadi Tanzania, bila wao kurudi Afrika Kusini.