Viongozi wa Soka nchini wametakiwa kuyaenzi yale yote mazuri yaliyofaywa na aliyekuwa mwekezaji na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Marehemu Yusuph Manji aliyefariki dunia Juni 29 jijini Florida Nchini Marekani alipokuwa akipatiwa Matibabu.

Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya yanga Frederick mwakalebela amezungumza juu ya uwekezaji wa Manji kunako Klabu hiyo licha ya misukosuko waliyokuwa wakipitia.

“Unapozungumzia Legacy ya baadhi ya viongozi wa Klabu ya Yanga African hususani wenyeviti wa klabu utakuwa ni mchoyo wa Fadhila usipomzungumzia Manji kwamba ni moja wapo ya watu waliokuwa kwenye nafasi ya juu sana kuweka Legacy ya kuweza kuiongoza Klabu ya Yanga, alikuwa ni mfadhili mkubwa ndani ya Yanga African na Yanga ilikuwa haina wa wafadhili kipindi kile lakini alijitahidi kwa kiasi kikubwa sana katika kuifanya Yanga isimame kwa kipindi kile, ” Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga SC – Frederick Mwakalebela.

Kwa upande wa usajii, Mwakalebela ameeleza kuwa Manji aliiwezesha Klabu hiyo kufanya sajili bora zaidi ambazo zimeendelea kuzungumzwa wakiwemo Kelvin Yondani, Emanuel Okwi na wengine wengi.


“Kama wanamichezo tukiangalia vitabu vya kumbukumbu zetu na vitabu vyetu tunaona kabisa kwamba Manji alikuwa ni moja ya watu ambao ameifanyia makubwa kabisa Klabu ya Yanga, ni msiba Mkubwa kwa sisi wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga hatuwezi kumsahau hasa katika kizazi kilichokuwepo katika utawala wa Manji, ”.

Mwakalebela ameongeza kwa kuwataka viongozi wa Klabu mbalimbali za soka ikiwemo Yanga kuyaenzi kwa vitendo yale yaliyokuwa yakifanywa na Manji pindi watakapoomba dhamana ya uongozi.

Kwa upade wake moja ya wachezaji waliokuwa wakihuduamu kunako Klabu ya Yanga enzi za uwekezaji wa Yusuph Maji, Said Juma Makapu ameeleza ni kwa jinsi gani Manji alikuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha wachezaji wanapambana huku akipongeza ukuaji wa Klabu hiyo kutoka uwekezaji wa Manji mpaka ulipo sasa Mkononi mwa GSM.

“Manji alikuwa na uwekezaji mzuri, tulichukua ubingwa mara tatu mfululizo juu ya uwekezaji yeye, wachezaji tulikuwa tunaishi maisha mazuri, tangu alipokuwepo Manji n ahata sasa walioshika kijiti naona mafanikio makubwa zaidi nah ii inaonyesha wazi kua uwekezaji wa sasa pia ni mzuri na naamini wanaendeleza pale walipoishia waliopita kwa kuhakikisha Yanga SC inazidi kukua zaidi, ” Amesema Said Makapu - Mchezaji

Yusuph Manji ambaye alizaliwa mnamo Oktoba 14 mwaka 1975 katika Jiji la Dar es salaam aliiongoza Klabu ya Yanga kwa miaka mitano akiingia madarakani mwaka 2012 na kujiuzulu mwaka 2017 ambapo anakumbukwa na wana Yanga kwa kutwaa mataji manne ya Ligi kuu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement