Victor Osimhen Nje Ya Uwanja Kwa Muda Akiuguza Majeraha
Mshambuliaji kimataifa wa Nigeria anyehudumu katika klabu ya SSC Napoli alipata majeraha kwenye msuli wa paja wakati akihudumu katika timu yake ya taifa.
Katika mchezo wa kirafiki wa 2-2 kati ya Nigeria na Saudi Arabia siku ya Ijumaa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alilazimika kuondoka kwenye mchezo huo akiwa na jeraha.
Tarehe ya kurejea kwa Osimhen haikuainishwa na Napoli, lakini majeraha kama hayo kawaida huchukua muda wa wiki nne hadi sita za kupona.