Mshambulizi wa Bayer Leverkusen na timu ya Taifa ya Nigeria Victor Boniface anaweza kukosa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2023 kutokana na jeraha.

Kulingana na vyanzo vya habari kambini, Boniface alipata jeraha la misuli katika mazoezi, lakini ukubwa wa jeraha hilo bado haujafahamika Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikosa mechi za kirafiki za Super Eagles dhidi ya Al Gharib na Guinea kutokana na jeraha hilo.


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement