Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amependekeza kutoa msamaha kwenye uingizaji wa mashine za ‘’VAR’’ na vifaa vyake kwa ufafanuzi utakaotolewa hapo baadaye akisema uamuzi huo utasaidia kuwa na ‘’VAR’’ za kutosha katika viwanja vyote Tanzania. 

Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni Jijini Dodoma leo June 13,2024.


 Waziri Mwigulu amesema yafuatayo “Kuhusu ubora wa eneo la kuchezea, yaani pitch kwenye viwanja mbalimbali, tayari Serikali ilitunga sheria inayotoa msamaha kwenye uingizaji wa nyasi bandia na vifaa vyake”

“Msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania tutaanza kutumia ‘’VAR’’ ili kuhakikisha matokeo yanayopatikana uwanjani yanakuwa ya haki maana kuna timu zimezidi msimu mmoja penati 10, halafu zikifungwa zenyewe magoli yanakataliwa” Mhe. Mwigulu Nchemba.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement