Uwanja mpya wa michezo utakaojengwa mkoani Arusha, unatarajiwa kupewa jina la Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika kipindi maalumu cha Wasafi Radio, jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema pendekezo hilo limebaki kwa Rais Samia kulipitisha.

“Tumependekeza hivyo kwa heshima ya mchango wa Rais Samia kwenye michezo, sanaa na utamaduni na Tanzania imefikia maendeleo makubwa,” amesema Msigwa.

Msigwa amesema uwanja huo unatarajia kuwa na uwezo wa kuingiza watazamaji 30,000 na utajengwa kwenye Kata ya Olmonti huko Arusha.

Eneo hilo kwa sasa linamilikiwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na lina ukubwa wa ekari 36.1. Msigwa amesema ujenzi huo wa uwanja ni sehemu ya jitihada za Tanzania kuandaa fainali za Afcon 2027 na zitafanyika kwa ushirikiano na nchi za Kenya na Uganda.

“Kama Rais Samia Suluhu Hassan atapitisha pendekezo letu, uwanja utakapokamilika utabeba jina lake," amesema Msigwa.

Aidha, Msigwa amesema "Viti vyote, jumla ya 60,000, vitabadilishwa na kuwekwa vipya. Ukarabati utakapokamilika, uwanja huo utakuwa umebadilika sana," amesema na kuongeza zaidi ya Sh31 bilioni zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo.

Mbali na Uwanja wa Benjamin Mkapa, uliopewa jina la Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Benjamin Mkapa, viwanja vingine vya michezo vyenye majina ya wakuu wa zamani wa wa nchi, ni Uwanja wa Kambarage, Shinyanga uliopewa jina la Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania, Hayati Julius Kambarage Nyerere na Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo Tabora, uliopewa jina la Rais wa Awamu ya pili, hayati Ali Hassan Mwinyi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement