Timu za APR FC na Rayon Sports ndizo zitakazokutana Jumamosi Juni 15,2024 katika ufunguzi wa Uwanja wa Amahoro baada ya kufanyiwa marekebisho.

Wizara ya Michezo imetangaza kuwa vilabu vyote viwili vimekubali kucheza mchezo huo ambao kiingilio itakuwa ni elfu moja na elfu kumi VIP kwa faranga za Rwanda.


Hata hivyo, timu hizi bado hazijaanza mazoezi kutokana na baadhi ya wachezaji kwenda likizo baada ya Ligi kumalizika na wengine katika timu za Taifa.

Rayon Sports ilimaliza Ligi ikiwa na wachezaji nane wenye mikataba huku APR FC ikiwa na wachezaji watano.

Uwanja wa Amahoro ambao utakuwa unapokea hata mechi za Kimataifa una uwezo wa kupokea watu 45,000 baada ya kufanyiwa marekebisho hayo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement