Kocha wa Atalanta, Gian Piero Gasperini ameeleza kuwa anauhakika na timu yake iko tayari kiakili na kimwili kukabiliana na timu ya Bayer Leverkusen katika fainali ya Ligi ya Europa hii leo.

Gasperini ameeleza wazi kuwa wanaamini kwamba wametayarisha kila kitu kuanzia kisaikolojia sambamba na kimwili hivyo kilichobaki na katika kupambana.

Mbio za Leverkusen za kutoshindwa msimu huu katika michuano yote zimewafanya wapewe jina la 'Neverlusen', huku mabingwa hao wa Bundesliga pia wakiwa wametinga fainali ya Kombe la Ujerumani ambapo watamenyana na FSK Jumamosi ya Mei 25 mwaka huu.

Gasrerini ameongeza kuwa wanafahamu kuwa wanakabiliana na timu kubwa na wanaamini hata matokeo ambayo wamepata msimu huu sio bahati mbaya lakini wanaamini katika Safari yao ambayo imewafikisha mpaka hatua hiyo ya Fainali.

Kwa upande wake Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso ameeleza kuwa Kujiamini kwao kunaendelea kuwasukuma na hawataki kusubiri hadi sekunde za mwisho za mchezo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement