Habari ya Bayern Munich kumteua Vicent Kompany kuwa kocha wao imeshtua watu wengi sana kwa kile kilichotokea kwenye Ligi kuu ya England katika msimu uliomalizika wa 2023/24 ambapo Burnley inayofundishwa na Kompany imekuwa miongoni mwa timu tatu zilizoshuka daraja sambamba na Sheffield United na Luton.

Uteuzi wa Kompany umeshtua wengi hivi karibuni, haikutegemewa timu kubwa kama Bayern Munich ambayo inaongoza kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Ujerumani ikifanya hivyo mara 33 huku ikichukua taji la Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara sita na lile la Super Cup Ulaya mara mbili.

Wengi walitegemea kuona Bayern Munich ingempa ajira hiyo kocha nwenye jina na wasifu mzuri ambaye ana uzoefu wa kutosha kutokana na ukubwa wa majina ya wachezaji waliomo katika kikosi hicho lakini wakaamua kuangukia kwa Kompany.

Uteuzi wa Kompany unaashiria kwamba Bayern Munich haikujikita katika kuangalia matokeo tu ambayo Burnley chini ya kocha huyu imeyapata katika msimu uliomalizika lakini walifanya tamthini ya kina ya vitu na vigezo vingi ambavyo mwisho wa siku vimekuja kuwapa majibu kuwa anayestahili ni nyota huyo wa zamani wa Manchester City badala ya wale ambao wengi walikuwa wanawapigia chapua hapo kabla.

Inawezekana tamthini yao imewapa jibu kuwa Kompany ni kocha mzuri ambaye ameangushwa na rasilimali alizonazo ndani ya Burnley lakini wakajiridhisha kwamba ndani ya Bayern Munich anaweza kuwapa matunda chanya kutokana na ubora wa wachezaji ambao anaenda kukutana nao.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement