USHINDI wa mabao 3-1 ambao Simba imeupata usiku wa Jumanne kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi dhidi ya Singida Fountain Gate umeifanya kupunguza tofauti ya pointi kati ya saba Yanga kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara kubaki saba

Awali, Yanga ambao walikuwa mbele kwa mchezo mmoja, walikuwa wakiongoza msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 10 baada ya kuichapa Ihefu SC jana Junatatu, mvua ya mabao 5-0 kwenye uwanja huo uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mabao ya Simba kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Sadio Ntibazonkiza katika dakika ya tano na tisa (amefikisha mabao saba) huku chuma ya tatu ikifungwa na Freddy Koublan dakika ya 34 huku la Singida FG likifungwna Thomas Ulimwengu dakika ya 84.

Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 42 na imeendelea kusalia katika nafasi ya tatu, wamezidiwa pointi ni mbili kati yao na Azam FC ambao wapo nafasi ya pili huku wakiwa mbele kwa michezo miwili.

Yanga ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 49 kileleni.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement