Cole Palmer alifunga mabao mawili ndani ya dakika za lala salama na kukamilisha hat-trick yake na kuipatia Chelsea ushindi wa ajabu dhidi ya Manchester United licha ya hapo awali kuwacha uongoza wa mabao mawili.

Hatua hiyo inajiri huku Liverpool wakiwashinda wageni wao Sheffield United 3-1 na kupanda hadi kilele cha ligi kuu ya England.

Bao la ushindi la hivi punde zaidi lililofungwa katika historia ya Premier League, katika dakika 100 na sekunde 39, liliwashangaza United, ambao walitangulia dakika tisa za majeruhi, na kupelekea Stamford Bridge kutapatapa.

United walikuwa mbele kwa dakika 99 na sekunde 17, ikiwa timu ambayo imewahi kuongoza katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza na kushindwa.

Mapigo hayo mawili ya dakika za lala salama yalimalizia mchezo ambao ulianza kwa kasi, huku nahodha wa The Blues, Conor Gallagher akiwaweka mbele wenyeji.

Ndani ya dakika 20 Palmer alifunga bao la pili la wenyeji baada ya Antony kumchezea vibaya Marc Cucurella.

Lakini Alejandro Garnacho aliamsha ushindi wa United alipoingilia kati pasi mbovu ya Moises Caicedo kwenye eneo la nyuma.

Bruno Fernandes aliisawazishia United dakika tano baadaye alipounganisha kwa kichwa krosi ya Diogo Dalot.

Garnacho alifunga la pili alipounganisha kwa kichwa krosi bora kutoka kwa Antony na kumpita kipa Djordje Petrovic, na kile ambacho United walidhani ndio washindi.

Mechi hiyo ilimalizika kwa kishindo huku Chelsea ikitwaa pointi zote tatu.















You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement