Uongozi wa klabu ya Yanga umeahidi kuongeza nguvu kwenye kikosi ili kuwa imara zaidi katika msimu ujao wa mashindano.

Rais wa Klabu ya Yanga Eng: Hersi ameeleza watakuwa wakifanya sajili za kuongeza uimara kwaajili ya msimu ujao huku wakihakikisha wale wanaowahitaji wanaendelea kubaki nao.

“Leo wachezaji wanaanza likizo zao, watakuwa na likizo ya mwezi mmoja, baada ya hapo tutakutana nao tena kwaajili ya kujiandaa kwa mashindano ya msimu ujao mwanzo mwa mwezi Julai wakati huo sasa tutakuwa tumeongeza uimara wa kikosi chetu, ” Amesema Rais wa Yanga SC – Eng: Hersi

“Tutakuwa tukifanya sajili za kuongeza uimara kwaajili ya msimu ujao na kuhakikisha wale ambao tunao na tunawahitaji hawataondoka, hilo ni jukumu kubwa sana ambalo tunalo, ” Amesema Rais wa Yanga SC – Eng: Hersi

Eng: Hersi ameongeza kuwa wamejipanga kupambana na fitna ambazo huwa zinatokana na Klabu kuwa na mafanikio na wanaamini pia wachezaji ambao ni sehemu ya mafanikio wapo imara.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement