Uongozi wa Klabu ya Singida Fountain Gate FC umekiri kuwa msimu uliopita wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara walishindwa kufikia malengo kutokana na wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa maana ya First Eleven kuondoka.

Afisa Habari wa Singida Fountain Gate FC Issa Mbuzi ameeleza juu ya mikakati yao kuhakikisha msimu ujao wa mashindano wanakuwa imara kwa kuhakikisha wachezaji watakaoondoka hawaachi athari kwa wanaobaki huku akigusia suala lao la madai sambamba na maboresho ya kikosi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement