Uongozi wa Klabu ya Pamba JIJI FC umeeleza kuwa kwa sasa ni wakati wa kusaka heshima mbele ya Mabingwa wa Ligi ya NBC Championship katika mchezo wa leo ukiwa ni maalumu kwaajili ya kumkabidhi Kombe la Ubingwa Ken gold kunako Dimba la Chamazi jijini Dar es salaam.

Afisa Habari wa Pamba Jiji FC, Moses Wiliam ameeleza kuwa Licha ya kwamba wanakutana na mabingwa lakini kikosi kipo tayari kupambana na wapinzani wao huku akigusia juu ya Klabu ambazo zimesalia na zinazopanda kushiriki NBC Championship kuhakikisha wanakuwa na ushirikiano wa karibu zaidi na TV3 kwaajili ya kuendelea kujitangaza.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement