Uongozi wa Klabu wa Mbeya kwanza umeweka wazi juu ya dhamira yao ya kupanda Ligi kuu msimu ujao wa 2024/25 ukiwa umebaki mchezo mmoja pekee wa kumaliza msimu wa Michuano ya NBC Championship.

Mwenyekiti wa Mbeya Kwanza Mohamed Mashango ameweka wazi kuwa licha ya kukwamisha kuwa katika nafasi za juu zaidi kama malengo yao yalivyokuwa hapo awali lakini kwa sasa wameshadhamiria kutumia nafasi waliyopo katika Ligi hiyo bila kujali uwiano wa pointi baina yao na wapinzani waliyo juu yao kwa maana ya Pamba wenye Pointi 61 wakishika nafasi ya pili huku wao na Biashara United wakiwa na Pointi 59.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement