Uongozi wa Klabu ya AIK Stockholm ya Sweden ambayo ipo nchini Tanzania kwa mwaliko wa Azam FC kwa ajili ya kujenga mahusiano na wenyeji umeupongeza uongozi wa Klabu ya Azam kwa kuendeleza na kukuza vipaji vya vijana ambao wanaamini watakuwa na faida kubwa kwa nchi hapo baadaye.

Akizungumza mara baada ya kutazama vipaji vya vijana wa timu ya U20, Mtendaji Mkuu wa AIK Stokholm, Fredrik Söderberg ameeleza kuwa kwa mtazamo wa nchi za Ulaya wanaona kuna vipaji vingi sana ndani ya Azam FC ambavyo wanaimani vikiendelea kuendeezwa itakuwa ni faida kwa Taifa.

Ugeni huo umeongozwa na mtendaji mkuu wa club hiyo (CEO), Fredrik Söderberg, Mkurugenzi wa Ufundi,(Technical Director)Peter Wennberg, na msaka vipaji mkuu, (Chief Scout)Tobias Ackerman.

Timu zaidi ya 10 kutoka akademi mbali mbali za mikoa tofauti hapa nchini zitashiriki, ambazo zina ushirikiano nazo Azam FC kufuatia makubaliano yaliyoingiwa mapema mwezi uliopita.

Mashindano hayo yatashirikisha wachezaji wa chini ya miaka 15, 17 na 20, umri chini ya na chini ya miaka 15 ambapo yameanza Aprili 30 na yatamalizika Mei 4 mwaka huu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement