UMRI PAMOJA NA PESA ZAITOA REAL MADRID KWENYE MBIO ZA KUMNASA KYLIAN MBAPPE
Real Madrid wamefutilia mbali uwezekano wa kumsajili nyota wa PSG Kylian Mbappe
Mbappe amekuwa akilengwa sana na Madrid katika miaka ya hivi karibuni, lakini wameamua kusitisha harakati zao za kumnasa mshambuliaji huyo.
Sababu ikiwa Mbappe atadai mshahara mkubwa angalau euro milioni 20 kwa mwaka na bonasi kubwa,
Sababu nyingine ni umri wake kwani Mbappe angekuwa na miaka 26 wakati anajiunga na Madrid na klabu ina nia ya kusajili wachezaji katika umri mdogo pia klabu inahofia kutumia pesa nyingi kumnunua kungesumbua mashabiki na kusababisha matatizo ya kiuchumi.