Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Korea Kusini amefukuzwa kazi kufuatia mzozo kati ya mchezaji nyota wa taifa hilo na nahodha Son Heung-min dhidi ya mchezaji mwenzake wa taifa hilo na kiungo tegemezi Lee Kang-in kabla ya timu hiyo kuondoka kwenye michuano ya kombe la Asia iliyomalizika hivi karibuni..

Taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Korea Kusini (KFA) Chung Mong-gyu ilisema akitangaza kocha Jürgen Klinsmann ameshindwa kuonyesha umahiri wake katika kusimamia mchezo, wachezaji, pamoja na uongozi thabiti uliotegemewa kwake kama kocha, "Uwezo wa Klinsmann na mitazamo yake haifikii namna Korea kama taifa imekuwa nayo.”

Hasira za Korea Kusini zimechagizwa na kufurumushwa bila mategemeo kwenye michuano ya Asian cup dhidi ya taifa dhaifu michezoni Jordan, hivyo ugomvi wa nahodha son na mchezaji mwenzake ukaja kuchochea zaidi kupotea kwa kibarua cha kocha Jurgen Klinsmann ambaje aliongoza taifa hilo kwa mwaka 2023 kisumu kwa miezi chini ya 12 pekee

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement