Staa wa soka Karim Benzema amefungua mashtaka ya jina lake kudhalilishwa dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, GĂ©rald Darmanin ambaye alimtuhumu kuwa na uhusiano na Kundi la Muslim Brotherhood ambalo limepigwa marufuku katika Nchi kadhaa zikiwemo Misri, Urusi na Saudi Arabia.

Oktoba 2023, Darmanin alitoa mtazamo wake huo baada ya Benzema kutumia ukurasa wake wa Twitter kuandika anaunga mkono watu wa Gaza kutokana na kuathiriwa na vita inayoendelea baina ya Israel na Hamas ambapo alieleza Watoto na Wanawake ni waathirika Wakubwa.

Benzema (36) ambaye anacheza soka Saudi Arabia alikanusha tuhuma za Darmanin na katika maelezo ya mashtaka yake amesema umaarufu wake unatumiwa vibaya kisiasa.

Hiyo si mara ya kwanza kwa Darmanin kumshambulia kwa maneno Benzema, aliwahi kufanya hivyo akidai aligoma kuimba Wimbo wa Taifa wa Ufaransa alipokuwa akiichezea timu hiyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement